المدة الزمنية 1:25

MKOA WA RUVUMA KUENDELEA KUTUMIA MFUMO WA STAKABADHI GHALANI KWA MAZAO YA SOYA NA UFUTA

بواسطة KUSINI NEWS
76 مشاهدة
0
0
تم نشره في 2021/06/26

WADAU wa kilimo na Ushirika kutoka wilaya zote mkoani Ruvuma wamekubaliana kuwa hakuna soya wala ufuta utakaonunuliwa na kutoka nje ya Mkoa wa Ruvuma bila kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani. Wamepitisha azimio hilo katika mkutano wa uendeshaji wa mfumo wa stakabadhi ghalani uliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge na kufanyika Ikulu Ndogo mjini Songea. Mkutano huo umewashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wakuu wa wilaya,makatibu tawala,wakurugenzi wa Halmashauri, wenyeviti wa Halmashauri,Mstahiki Meya,viongozi wa vyama vikuu vya ushirika vya SONAMCU na TAMCU,Mwakilishi kutoka Bodi ya Leseni ya stakabadhi ghalani,maafisa kilimo na watumishi wengine. “Tumekubaliana wote kwenye kikao hiki,hivyo mkasimamie,hakuna soya wala ufuta utakaonunuliwa kutoka nje ya Mkoa bila kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani’’,amesisitiza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma. RC Ibuge ameziagiza Halmashauri na wilaya zote mkoani Ruvuma kusimamia kikamilifu utekelezaji huo na kuongeza kuwa Halmashauri zina jukumu la kuunda na kuhuisha Kamati za usimamizi wa stakabadhi ghalani ili kutatua changamoto ndogo ndogo za wadau. Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma pia ameagiza elimu endelevu kuhusu taratibu,sheria na miongozo iliyopo katika mfumo wa stakabadhi ghalani ianze kutolewa kila Halmashauri na kwamba vyama vya ushirika vinahusika zaidi ili wadau wapate uelewe wa kina kuhusu umuhimu wa mfumo huo. Mfumo wa stakabadhi ghalani katika mazao ya soya na ufuta mkoani Ruvuma,umekuwa msaada katika kuwapatia wakulima kipato kikubwa ambapo takwimu zinaonesha kuwa msimu wa mwaka 2018/2019 kiasi cha tani 2,855.38 za soya na tani 8,428.27 za ufuta ziliuzwa kupitia mfumo huo na kwamba mwaka 2019/2020 tani 1,499.8 za soya na tani 12,234.76 za ufuta ziliuzwa.

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 0