المدة الزمنية 41:30

Salama Na Profesa ep 55 | MAPINDUZI HALISI Part 1

بواسطة YahStoneTown
108 916 مشاهدة
0
1 K
تم نشره في 2021/02/27

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #0762797291 Support us through https://anchor.fm/yahstonetown/support SUBSRIBE TO OUR CHANNEL https://bit.ly/YahStoneTownSubs Listen our Podcast on Spotify Link https://spoti.fi/2Uxr6Cm� �� ‪ApplePodcast Link https://apple.co/2Ou1bru� �� GooglePodcast Link https://bit.ly/GooglePodcastSalamaNa Audiomack Link https://bit.ly/YahStoneTownAudioMack ‪YouTube Link http://bit.ly/YoutubeSalamaNa Joseph Haule ni mmoja ya binadamu ambao nawapenda sana kwenye dunia hii na huwezi kuamini hata yeye anajiskia hivyo juu yangu, nikiwa naye vibe na story zetu huwa zinabamba sana. Kuanzia story za maisha, muziki, historia na hata kuwacheka watu wakati mwengine, ndo zetu. Nakumbuka baada ya kumsaka asubuhi moja hivi na yeye kutodaka simu (ambayo baadae aliniambia alimpigia Sallam simu akidhani yeye ndo aliyempigia badala ya Salama), hayo maelezo niliyapata baada ya yeye kukutana na tweet ya kulalamika kwangu juu ya yeye kutorudisha simu yangu. Tumetoka mbali kiasi chetu, mkubwa kwangu kwa miaka 7 na heshima yangu kwake si ya kupima kwa kisoda. Unaweza ukawa unajiuliza sasa mbona hatukuoni naye na mambo kama hayo (hiyo mambo kama hayo nimeongea kama yeye) well... Urafiki wetu si ule wa kugandana kama kifungo na shati, au kichwa na nywele au kucha na kidole ndugu yangu, urafiki wetu ni ule wa kuendeleza pale tulipoishia na kuangalia na kwa mbali juu ya kitu mwenzio anafanya huku tukitakiana Kheri. Nakumbuka vizuri mara yangu ya kwanza kukutana na Profesa, enzi za Times FM kule mjini, kipindi hiko mimi ndo nimepata ajira yangu ya kwanza na yeye ndo alikua Msanii wa mooto sana, hard blasters wako na moto wa tipa, na nani ndo kiongozi wa nyika? Nigga Jay. Urafiki wetu ulianzia hapo, na mpaka leo tunamshkuru Mungu. Ukuaji wake hasa ndo nia na madhumuni ya mimi na wenzangu kuona Prof atatufaa sana kumalizia episode yetu ya 55 na ngwe ya kwanza ya kazi yetu hii. Zaidi kama tujuavyo, hakuna msanii hata mmoja ambaye hajawahi kuvutiwa na hustle zake za kuanzia juzi mpaka leo hapa tulipo. Na hiyo inajumuisha kipaji na UANDISHI ulosimamia kucha. Jay tunakuzimia indeed! So wapi haya yoooote yalianzia? Mpaka sasa Mbunge nje ya Bunge? Well... Hata mbuyu ulianza kama mchicha, humu Prof anazungumza na sisi juu ya masuala ya familia na safari alizopitia, mikoa aliyowahi kuishi, mahusiano kati ya Marehemu Baba yake na Mama yake, wadogo zake, Kaka na Dada zake, elimu yake, experience yake mjengoni, nini maana ya baadhi ya vitu na mambo aliyowahi kuyapitia. Pia tuliongelea kupatikana kwa binti yake pekee Lisa, jinsi alivyokutana na mke wake, kipaji chake, kwanini Mikumi na kwa mbaaali uchaguzi mkuu uliopita. Profesa ni mwana flani ivi ambaye toka zamani ramani ya mambo yake yako mfuko wa nyuma, kupotea au kupoteza malengo si jambo rahisi kwake, labda kuchelewa tu kwa hayo aloyapanga. Na hivi sasa kwa miaka mitano hii ambayo yuko nje ya bunge, pengine ndo wakati wetu wa kufaidi kipaji chake na kuokota mawili matatu kwa wale wote tunao muangalia na kupenda nyenendo zake. Tafadhali enjoy. Love, Salama. Soundtrack Yeah by @MarcoChali /watch/QLnf4BH1euC1f Follow: Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown Channel Administered by Slide Digital Instagram: www.instagram.com/slidedigitaltz

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 163