المدة الزمنية 1:2

Bao la 'Feitoto' lililoipa Yanga pointi tatu dhidi ya JKT Tanzania (TPL - )

بواسطة Azam TV
18 643 مشاهدة
0
55
تم نشره في 2019/02/10

Goli pekee lililofungwa na kiungo Feisal Salum ‘Feitoto’ dakika ya 27, limeipa Yanga ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga. Feisal amefunga goli hilo akimalizia pasi ya Gadiel Michael kutoka winga ya kushoto na kuwafanya mabingwa hao wa kihistoria wa ligi hiyo kuondoka na alama tatu muhimu zinazowafanya kujikita kileleni kwa kufikisha pointi 58 mbele ya Azam FC yenye pointi 48 na Simba yenye pointi 36. Matokeo haya pia yanawapoza machungu Yanga kutokana na matokeo ya michezo mitatu iliyopita ambayo hawakupata ushindi wakifungwa mchezo mmoja na kutoka sare michezo miwili.

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 4