المدة الزمنية 4:36

Watu Watano Wahukumiwa Kunyongwa kwa kosa la Mauaji Njombe

بواسطة NJOMBE TV
7 963 مشاهدة
0
25
تم نشره في 2021/10/22

Mahakama Kuu Kanda ya Iringa imewahukumu kunyongwa hadi kufa washitakiwa watano baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la mauaji. Hukumu hiyo imesomwa na Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, Jose Mlyambina na katika mashitaka matatu ya mauaji aliyoendesha, shauri namba namba 56 ya mwaka 2016 ambalo washitakiwa Shaibu Putika mwenye ummri wa miaka 37 na Christopher Kahewanga mwenye umri wa miaka 41, wote kwa pamoja wametiwa hatiani kwa kushiriki kutenda kosa la mauajii ya Chance Putika kwa kukusudia kinyume na kifungu cha 196 na 197 cha Kanuni ya Adhabu Marejeo ya 2019. Tukio hilo linatajwa kutendeka tarehe 15 Mei, 2016 katika Kijiji cha Peru handa kilichopo Wilaya na Mkoa wa Njombe . Jaji Mlyambina ameeleza kuwa Mshtakiwa wa kwanza Shaibu Putika alimtafuta mshtakiwa wa pili Christopher Kahewanga ambaye walikubaliana kwa malipo ya Tsh. laki tatu ili waweze kushirikiana kumuua Chance Putika ambaye ni mdogo wa Shaibu Putika anaelezwa kuwa alikuwa na matatizo ya kiakili. Shauri lingine ni Shauri namba 53/2017, Mahakama Kuu kand ya Iringa kupitia Jaji Jose Mlyammbina imewahukumu washitakiwa watatu kunyongwa hadi kufa ambao ni Athony Magehema (miaka 28), Titho Nzota (miaka 34) na Emmanuel Magehema (miaka 27) baada ya kukutwa na hatia ya kumuua Hilda Kinanilo katika kijiji cha Igominyi wilaya ya Njombe kinyume na kifungu cha 196 na 197 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2019. Tukio hilo limetajwa kutendeka tarehe 28 Machi mwaka 2016 katika Kijiji cha Igominyi wilaya na Mkoa wa Njombe ambapo washitakiwa wanatajwa kumuua kwa kumchoma moto Hilda Kinanilo wakitumia mafuta ya petroli. Mawakili wa serikali Matiku Nyangero na Andrew Mandwa wameieleza mahakama kuwa washtakiwa walimfuata Hilda Kinanilo nyumbani akiwa na mume wake na kuanza kuwakimbiza, ambapo mumewe Angelius Mayemba alifanikiwa kukimbia lakini kwa isiyobahati mkewe Hilda Kinanilo alikamatwa na washitakiwa hao wanaodaiwa kumchoma moto na kumsababishia umauti. Njombe imekuwa ikitajwa mara kwa mara katika matukio mbalimbali ya mauaji ambayo kwa asilimia kubwa yamekuwa yakihusishwa na imani za kishirikina. Hata hivyo bado jeshi la Polisi mkoa wa njombe linaendelea na jitihada za kuelimisha jamii kuachana na imani za kishirikina ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua kali wale wote wanaojichukulia sheria mkononi.

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 8