المدة الزمنية 4:43

Jifunze kutengeneza chakula cha samaki na vijue vifaa vya kufugia samaki

بواسطة MKULIMA SMART TV
4 349 مشاهدة
0
40
تم نشره في 2021/05/29

CHAKULA CHA SAMAKI WA KUFUGWA KWENYE MABWAWA ufugaji wa samaki kwa mtaji mdogo ufugaji wa samaki kambale chuo cha ufugaji wa samaki chakula cha samaki ufugaji wa samaki dar es salaam ufugaji wa samaki katika eneo dogo changamoto za ufugaji wa samaki ufugaji wa samaki kwenye pipa Ni muhimu sana kwa mfugaji kuweza kupata au kutengeneza chakula kilichobeba virutubisho vyote muhimu ambavyo vitasaidia samaki katika ukuaji wake. Wakati wa kutengeneza chakula, ni vyema mfugaji kuhakikisha chakula hicho kinakuwa na virutubisho vifuatavyo; protini (kiini lishe), wanga, mafuta (fat /lipid), vitamini na madini. Viritubisho hivyo vitano ni muhimu kwa samaki kwa sababu kila kimoja kina kazi yake ndani ya mwili wa samaki husika ambaye anafugwa. Chakula cha samaki hutengenezwa kulingana na aina ya samaki husika, mfano kuna samaki aina mbalimbali kama Sato, Pelege, Sehewa, Mwatiko, Kambale mchanganyiko wake huwa tofauti tofauti. Muongozo huu ni maalumu kwa ajili ya samaki aina Tilapia (Sato, Pelege). Mahitaji • Unga wa dagaa (Fish meal) protini ya mnyama. Uwe umesagwa na kuwa kwenye hali ya ungaunga (powder form). Kazi kubwa ya protini hii ni kufanya mwili kukua vizuri. Protini hii huitajika kwa wingi zaidi hasa kipindi ambacho samaki huwa mdogo na katika rika la samaki mzazi. • Soya lishe (Soya bean) protini ya mmea. Hii ni aina ya protini ambayo hufanya kazi ya kuimarisha mwili na kukua kwa samaki vizuri. Protini hii hupatikana katika mimea jamii ya mikunde kwa kuchemsha kidogo kisha kuzianika mpaka zikauke halafu kuzisaga ili ziwe kwenye hali ya unga unga. Hutumika kwa wingi katika chakula cha samaki anapo kuwa mdogo sana na kipindi anachofikia kuwa mzazi (broder fish). • Pumba za mpunga, pumba za mahindi (rice bran, maize bran). Hiki ni chakula jamii ya wanga (carbohydrate) ambacho hufanya kazi ya kuongeza nguvu ndani ya mwili wa samaki. Pumba lazima ziwe zimesagwa vizuri na kuwa katika hali ya unga unga ili kumpa nafuu samaki katika ulaji wake. Huchanganywa na vyakula vingine zaidi katika kipindi ambacho samaki yupo katika rika la kati (grow out). Tunapendekeza kuanza kutumia pumba za mpunga kwani ni nzuri zaidi ila kama hazipatikani unaweza pia kutumia pumba za mahindi. • Unga wa mhogo,unga wa ngano (cassava flour, wheat flour). Hii nayo ni aina mojawapo ya chakula aina wanga ambayo husaidia katika kumpa samaki nguvu ndani ya mwili wake. Kazi nyingine husaidia kuviunganisha virutubisho vyote kuwa kwenye sehemu moja (single compound) hivyo humfanya samaki kula virutubisho vyote kwa wakati moja. Wataalamu wanapendekeza kuanza kutumia unga wa mhogo ila kama haupatikani basi unaweza kutumia unga wa ngano. • Machicha ya nazi, mashudu ya alizeti (Copra meal, sun flower cake). Hii ni aina mojawapo ya virutubisho aina ya mafuta ambayo hufanya kazi ya kunenepesha mwili wa samaki vizuri. • Vitamin mineral mix, premix na D.I. Grow. Mbinu mpya ya kufuga samaki bila vidimbwi SAMAKI ni lishe miongoni mwa Wakenya wengi; aidha wafanyabiashara wamekuwa wakijipatia kipato kizuri kwa kufanya biashara ya samaki. Mbali na samaki kutumika kutengeneza vitoweo mbalimbali pia huunda sampuli ya mafuta yanayotumika kama lishe kwa watoto. Biashara ya kufuga samaki ina faida nzuri kwa sababu soko lake ni pana na wala sio la kuhangaika, muradi mkulima azalishe samaki wa kutosha. Badala ya kutegemea vidimbwi na mabwawa kama ilivyofanywa na wafugaji siku za mbeleni, uvumbuzi mpya umefanya ufugaji wa samaki kuwa rahisi ikiaminika kuwa changamoto sio upatikanaji wa maji bali kufanya shughuli nzima ipasavyo. Unayachukua mayai ya samaki kisha yakachanganywa na chembe chembe za uzalishaji kutoka kwa samaki wa kiume, ambao huchukua masaa 48 kuzalisha samaki wadogo (fingerlings). Samaki wadogo huchukua siku tano kabla ya kulishwa vyakula vya kawaida vilivyochanganywa na unga na viungo muhimu vya majani. “Ujuzi wa kufuga samaki niliupata mtandaoni, ndio maana nikaishawishi shule kukumbatia mtindo huu wa kisasa ili kuzalisha samaki kwa ajili ya kutoa mafunzo ya kitaalam kwa nwanafunzi na kutosheleza mahitaji ya shule,” akasema Wangare. Ufugaji wa samaki kupitia mbinu za kisasa unaweza kusaidia kwenye utunzaji wa mali asili, pasipokuwa na uchafuzi wa maji wala mazingira wanamokulia viumbe hawa Fangasi Ugonjwa mkubwa unaosumbua samaki ni ule wa fangasi ambao hutokana na maji machafu, magamba huanza kumtokea samaki. Ili mfugaji aweze kuanza ufugaji wa samaki ni muhimu kupata kibali cha matumizi ya maji kwa mfano kupata kibali kutoka kwa serikali kwa sababu samaki ni tofauti na wanyama wengine. “Samaki anaishi kwenye maji anakula kwenye maji na anategemea kila kitu kwa mujibu wa maji yanayopatikana,” aliongezea. Ili mkulima aweze kufuga samaki kibiashara mkulima anahitaji kuwa na mabwawa takriban sita ili uvunaji wa samaki usipunguze upatikanaji wa bidhaa hii muhimu sokoni.

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 4