المدة الزمنية 8:19

Je Dalili za Mimba ya Mapacha pekee hutosheleza kuonesha kuwa Una Mapacha Tumboni | Nini ufanye

بواسطة Dr. Mwanyika
27 724 مشاهدة
0
310
تم نشره في 2021/11/26

Jinsi ya kupata Mapacha Jinsi ya kupata Mimba ya Mapacha Mimba ya Mapacha Mapacha, Mapacha, Mapacha Dalili za Mimba ya Mapacha Dalili ya Mapacha Dalili za Mimba ya Mapacha huweza kuashiria kuwa una Mimba ya Mapacha, Lakini ikumbukwe kwamba Dalili za Mimba hiyo pekee hazitoshelezi kuweza kuonesha wazi kuwa una Mimba ya Mapacha kwa asilimia 💯. Hii ni kwa sababu wakati mwingine Dalili hizo hufanana na Aina nyingine ya Mimba mfano; Mimba Zabibu au hata Mimba ya Mtoto mmoja tuu Tumboni mwako. Hivyo unahitaji kufanya Ultrasound ili kuweza kujua kama una Mimba ya Mapacha na hii huweza kukupa majibu kwa asilimia 💯. Jinsi ya kupata Mapacha Jinsi ya kupata Mimba ya Mapacha Mimba ya Mapacha Mapacha, Mapacha, Mapacha Dalili za Mimba ya Mapacha Dalili ya Mapacha Unaweza kufanya Ultrasound katika Vipindi tofauti tofauti katika kipindi cha Ujauzito mfano; 1. Miezi Mitatu ya Mwanzoni mwa Ujauzito. 2. Miezi Mitatu ya katikati wakati wa Ujauzito. 3. Miezi Mitatu ya Mwishoni mwa Ujauzito. Dalili za Mimba ya Mapacha ni Kama hizi zifuatazo; 1. Kutapika au kuona kichefu chefu asubuhi (Morning Sickness) huwa ni zaidi ukilinganisha na wale wenye mimba ya kawaida. Kumbuka kama Mama mjamzito ni Mara ya kwanza kuwa mjamzito au mimba ya kwanza au hata kwa wengine kuna magonjwa mengine mfano kutapika wakati wa ujazito (Hyperemesis Gravidarum) huwa na Dalili hizo pia 2. Kuchoka mara kwa mara na zaidi hii ni kutokana na mabadiliko ya kimwili na homoni za mwanamke wakati wa ujauzito lakini pia kwa sababu ya uzito mkubwa wa watoto wawili. 3. Kuanzi wiki ya 16 Mama ambaye aliwahi kuwa na mimba miaka ya nyuma ataona watoto wanacheza mara nyingi zaidi kuliko kawaida. 4. Kuongezeka kwa uzito wa Mama kwa kasi zaidi na kuwa na uzito mkubwa kuliko Mama mwenye Mimba ya kawaida, kwa kawaida uzito huongezeka kwa wastani wa (11-25)kg kwa kipindi chote cha mimba kwa akina mama wenye uzito wa kawaida wanapokuwa na ujauzito hivyo basi, Kumbuka magonjwa ya shinikizo kubwa la damu (Gestational hypertension, Preeclampsia na Eclampsia) huweza kuwa na Dalili hii za kuongezeka kwa uzito mkubwa hivyo ukifikisha miezi mitano hakikisha unajua presha yako na ujiridhishe kuwa ni ya kawaida. 5. Tumbo kuongezeka ukubwa kuliko umri wa mimba,hii ni kwa sababu ya uwepo wa watoto wawili tumboni,kumbuka siyo Mara zote tumbo la mama mjamzito kuongezeka kwa kasi zaidi kuliko kawaida ina maanisha kuwa mimba ya mapacha wakati mwingine huwa kuna magonjwa(Gestational Trophoblastic Diseases,Polyhydromnios/Hydromnios) ambayo huweza kuwa na Dalili hii pia kwa hiyo usijichanganye. 6. Kukosa pumzi Mara kwa Mara na zaidi, Hii ni kwa sababu ya ukuaji wa mfuko wa Uzazi wenye watoto wawili ndani yake na kusukuma misuli inayohusika na upumuaji iitwayo Diaflamu kwenda juu na kuingilia mwenendo wa Upumuaji. 7. Maumivu ya Nyonga na Mgongo Kutokana na Uzito mkubwa katika tumbo la Mjamzito mwenye Mimba ya Mapacha. Jinsi ya kupata Mapacha Jinsi ya kupata Mimba ya Mapacha Mimba ya Mapacha Mapacha, Mapacha, Mapacha Dalili za Mimba ya Mapacha Dalili ya Mapacha Nifuatilie kwenye channel yangu kuhusu Mambo ya Ujauzito. /c/DrMwanyika Nifuatilie Instagram kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://www.instagram.com/dr._mwanyika/ Nifuatilie kwenye website hii kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://mamaafya.com/ Nifuatilie kwenye Facebook page kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://www.facebook.com/JapideAfya/ Usisahau kudownload app ya Mama Afya Bora kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://play.google.com/store/apps/details?id=com.wapnum.mamaafyaapp ©Dr.Mwanyika #drmwanyika #mamaafya #MimbaMapacha

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 128