المدة الزمنية 7:53

KAMATIYA ULIZI NA USALAMA WILAYA NYAMAGANA YARIDHISWA UNAOTEKELEZWA NA KAMPUNI YA JR.INTERNATIONAL.

بواسطة Zepha mandia
138 مشاهدة
0
3
تم نشره في 2020/02/17

Serikali imekamilisha mradi mkubwa wa maji wenye gharama ya zaidi ya Tsh. Bilioni 38, utakaoanza kutoa huduma ya maji safi kwa wananchi wa mkoa wa Mwanza, waliokuwa wakikabiliwa na upungufu wa maji safi na salama kwa muda mrefu. Taarifa ya kukamilika kwa mradi huo, imetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (Mwauwasa) Mhandisi Leonard Msenyere, wakati wa ziara ya mkuu wa wilaya ya Nyamagana DK. Philis Nyimbi ya kutembelea tanki la maji la Nyegezi. Kaimu mkurugenzi wa mamlaka hiyo Mhandisi Msenyere, amesema mradi huo uliopo Kata ya Nyegezi tanki lake lina ujazo wa lita milioni 1.2, ambalo limejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 3.2, na utatoa huduma kwa kata tatu za mkuyuni, buhongwa na Nyegezi. Mnandi Mruto ni Mkurugenzi wa miradi wa kampuni ya ujenzi ya JR international, amesema kuwa kazi ya ujenzi wa matanki sita ya maji katika maeneo ya Nyegezi, Bugarika, Kitangiri, Nyamhongoro na nyasaka, ilikuwa ikifanyika usiku na mchana ili kuhakikisha inakamilika. Kisha DK. Philis Nyimbi, akaeleza kuwa kukamilika kwa mradi huo ni mpango wa serikali ya awamu ya tano wa kumtua ndoo kichwani mwanamke, na kwamba itasaidia wanawake kufanya shughuli za maendeleo badala ya kuamka usiku wa manene kusaka huduma ya maji. Januari 8 mwaka huu Naibu waziri wa maji Jumaa Aweso, alipofanya ziara mkoani Mwanza. alitoa wiki mbili kwa mkandarasi wa mradi huo JR International, kuhakikisha anakamilisha mradi huo ambao tayari umeanza kutoa maji.

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 0