المدة الزمنية 54:00

KKKT USHARIKA WA KIJITONYAMA IBADA YA MORNING GLORY

5 297 مشاهدة
0
97
تم نشره في 2021/04/29

KKKT USHARIKA WA KIJITONYAMA IBADA YA MORNING GLORY 29/4/2021 UJUMBE WA LEO : HAUTAFIA JANGWANI YOU'LL NEVER DIE IN THE DESERT Warumi 10 : 8 - 10 Kutoka 14 : 10 - 14 Isaya 43 : 18 - 19 Mithali 23 : 7a Zaburi 66 : 18 - 19 Warumi 10 : 8 - 10 8 Lakini yanenaje? Lile neno li karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo. 9 Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. 10 Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Kutoka 14 : 10 - 14 10 Hata Farao alipokaribia, wana wa Israeli wakainua macho yao, na tazama, Wamisri wanakuja nyuma yao; wakaogopa sana; wana wa Israeli wakamlilia Bwana. 11 Wakamwambia Musa, Je! Kwa sababu hapakuwa na makaburi katika Misri umetutoa huko ili tufe jangwani? Mbona umetutendea haya, kututoa katika nchi ya Misri? 12 Neno hili silo tulilokuambia huko Misri, tukisema, Tuache tuwatumikie Wamisri? Maana ni afadhali kuwatumikia Wamisri kuliko kufa jangwani. 13 Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa Bwana atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele. 14 Bwana atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya. Isaya 43 : 18 - 19 18 Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani. 19 Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani. Mithali 23 : 7a 7 Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo. Akuambia, Haya, kula, kunywa; Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe. Zaburi 66 : 18 - 19 18 Kama ningaliwaza maovu moyoni mwangu, Bwana asingesikia. 19 Hakika Mungu amesikia; Ameisikiliza sauti ya maombi yangu. Mhubiri : Mwl. Renald Mlawi Kwa maombi na ushauri: Mch. Dkt. Eliona Kimaro. Simu :+255655516053, +255754516053 YouTube : Rev. Dr. Eliona Kimaro TV Barua Pepe: elionakimaro555@gmail.com

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 33