المدة الزمنية 5:36

Kitendawili Kifo cha Kada wa CHADEMA Mwanza, Ndugu na Marafiki Wadai Majibu

بواسطة The Chanzo
712 مشاهدة
0
5
تم نشره في 2021/11/25

Kufuatia hatua ya kupotea na kupatikana akiwa amefariki kwa Erasto Amos Makaranga, aliyekuwa mwenezi wa CHADEMA Kata ya Buswelu, wilaya ya Ilemela, mkoani Mwanza, The Chanzo imefanya mazungumzo na ndugu wa Erasto kufahamu tukio hilo wamelipokeaje na hatua ambazo wangependa kuona mamlaka husika inazichukua. Tulizungumza pia na viongozi wa CHADEMA katika Kata ya Buswelu ambao wametueleza namna wanavyomfahamu Erasto Amos Makaranga na namna wanavyolichukulia tukio zima la kupotea na kuuwawa kwake. Wote, ndugu wa Erasto Amos Makaranga na viongozi wenzake wa CHADEMA, wameeleza kusikitishwa kwa tukio hilo lililomfika mpendwa wao, na kutoa wito kwa mamlaka husika kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo na kuhakikisha umma unaelezwa ukweli juu ya kile kimetokea. #TheChanzo

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 0