المدة الزمنية 9:15

KWA NINI MATITI HUUMA/KUWASHA KWA MJAMZITO | SABABU ZA MATITI KUUMA KWA MJAMZITO

بواسطة Dr. Mwanyika
24 711 مشاهدة
0
188
تم نشره في 2022/01/08

MAUMIVU YA MATITI KATIKA KIPINDI CHA UJAUZITO. Baadhi ya Wanawake hupata Maumivu ya Matiti ktk kipindi cha Ujauzito. Dalili hii huaanza kutokea Mimba inapofikisha Wiki 2 za Ujauzito kipindi ambacho Baadhi ya akina Mama Wajawazito huwa hawajajigundua kuwa wao ni Wajawazito na pia huendelea kuwepo kwa Miezi Mitatu ya Mwanzoni mwa Ujauzito huweza kupungua Miezi Mitatu ya katikati mwa Ujauzito na Kujitokeza Tena Miezi Mitatu ya Mwishoni mwa Ujauzito. Tafiti zinaonesha Wajawazito 17 Kati ya Wajawazito 100 huwa na Dalili hii ya Maumivu ya Matiti ktk kipindi cha Ujauzito. Maumivu ya Matiti ktk kipindi cha Ujauzito hutofautiana kati ya Mjamzito Moja na Mwingine kuna baadhi huwa na Maumivu kidogo na wengine huwa na Maumivu Makali zaidi mpaka kushindwa kufanya kazi zao za kawaida bila Matibabu. Hali hii huweza kujitokeza kwenye Titi au Ziwa Moja au Matiti yote Mawili. DALILI ZA MAUMIVU YA MATITI KATIKA KIPINDI CHA UJAUZITO. Mjamzito mwenye Hali hii huwa na Dalili zifuatazo; 1. Maumivu ya Matiti au Titi moja ambayo huwa kama Sindano zinachoma choma. 2. Maumivu Makali wakati wa Kujishika Matiti au Titi liloathirika. 3. Matiti kuongezeka Msisimko ambao si wa kawaida. 4. Maumivu kama Maumivu ya Kidonda kwenye Ziwa au Matiti yote Mawili. 5. Maumivu huweza kuuma kwenye Chuchu au Kuuma kuelekea kwenye Kwapa katika upande ambao Ziwa au Matiti yanauma. VISABABISHI VYA MATITI KUUMA KTK UJAUZITO. 1. Ongezeko la Homoni ya Estrogeni na Progesterone hususani kwenye Miezi Mitatu ya Mwanzoni mwa Ujauzito. Katika kipindi cha Mwanzoni mwa Ujauzito Kutokana na Ongezeko la Homoni ya Estrogeni hupelekea kuongezeka kwa Mishipa ya Damu na Vimirija vya Maziwa hali hii hupelekea Maumivu kwa Mjamzito. Kuna Baadhi ya Wanamke huweza kupata hali hii Siku chache kuelekea Hedhi yao ya kawaida ni Kutokana na Ongezeko la hizi Homoni za Progesterone na Estrogeni. 2. Ongezeko la Homoni ya Prolactin na Oxytocin ambazo hutolewa na Tezi ya Pituitari kwenye Miezi Mitatu ya katikati na Mwishoni mwa Ujauzito ambazo huuanda Mwili na Matiti kwa ajili ya utengenezwaji wa Maziwa ya Mtoto hupelekea Baadhi ya mabadiliko na Kuongeza kwa Mirija ya Maziwa kwenye Matiti na kupelekea Maumivu ya Matiti ktk kipindi cha Mwishoni mwa Ujauzito. 3. Uvaaji wa Brazia zisizobana na kushikiza Matiti vizuri. Matumizi ya Brazia ambazo si za Wajawazito kwenye kipindi cha Ujauzito huweza kupelekea Ongezeko kubwa la Maumivu ya Matiti kwa sababu hushikiza vibaya Matiti na kuachia sehemu nyingine za Matiti zikining'inia Vibaya na kupelekea Maumivu ya Matiti ktk kipindi cha Ujauzito. Hususani kwa Wajawazito wenye Matiti Makubwa Sana. MAMBO YAKUFANYA ILI KUPUNGUZA MAUMIVU YA MATITI KATIKA KIPINDI CHA UJAUZITO. 1. Vaa Brazia Nzuri zilizotengenezwa na Pamba ambazo zina Mikanda Mipana ya mabega na zinazoshikiza Maziwa au Matiti vizuri bila kuachia Baadhi ya sehemu za Matiti kwa Nje na kufanya Matiti kuning'inia, hii huweza kusaidia kupunguza Maumivu ya Matiti ktk kipindi cha Ujauzito, NB; Hususani kwa Wajawazito wenye Matiti Makubwa Sana. 2. Acha Tabia ya Kujishika Maziwa/Matiti au Kukamua Maziwa/Matiti yako kipindi ambacho yanakuwa yanauma, Kitendo Cha Kujishika shika Matiti hupelekea inflamesheni na Maumivu kuongezeka katika kipindi chako Cha Ujauzito. NB: Hii unapaswa kumwambia na mwenza wako ili aelewe Kitendo Cha Kushika Matiti huongeza hali ya Maumivu katika Kipindi cha Ujauzito kwa Mjamzito mwenye Maumivu ya Matiti ktk Ujauzito wake. 3. Unaweza kukanda Matiti yako kwa Maji ya Barafu na Kitambaa laini au Barafu ili kupunguza Maumivu ya Matiti ktk kipindi chako Cha Ujauzito na Endapo Maumivu yanazidi unatakiwa kuwahi hospitali kwa ajili ya Kuonana na Daktari na kuandikiwa Dawa za Maumivu. 4. Unatakiwa kuonana na Daktari endapo unapata Maumivu ya Matiti na pia unaona au kuhisi Dalili zifuatazo; Matiti kutoa Uchafu wenye harufu Mbaya au Damu, Uvimbe kwenye Matiti yako, Kujikunja kwa Ngozi ya Titi kwa Kuingia au Chuchu kuingia Ndani kusiko kawaida, Kubadilika rangi ya Ziwa kuwa Nyekundu au Njano kama Chungwa. Nifuatilie kwenye channel yangu kuhusu Mambo ya Ujauzito. /c/DrMwanyika Nifuatilie Instagram kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://www.instagram.com/dr._mwanyika/ Nifuatilie kwenye website hii kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://mamaafya.com/ Nifuatilie kwenye Facebook page kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://www.facebook.com/JapideAfya/ Usisahau kudownload app ya Mama Afya Bora kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://play.google.com/store/apps/details?id=com.wapnum.mamaafyaapp #MatitiKuuma #DrMwanyika #MamaAfya

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 131