المدة الزمنية 34:22

JPM AELEZA DIRA YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO AFUNGUKA JUU YA MAENDELEO LUKUKI.

بواسطة MNZAVA TV
41 مشاهدة
0
1
تم نشره في 2020/10/24

#AUBIRI AMANI ..AWATAKA WATANZANIA KUTII MAAGIZO YA NEC NA KUWATAKA WASIYUMBISHWE NA WATU WANAOJIPANGA KUIPOTEZA AMANI Mhe. Magufuli amewaomba wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro kumpa ridhaa ya kuwaongoza kwa miaka mitano tena sambamba na kuyatathimini mambo muhimu yaliyotendeka katika awamu ya tano ikiwemo huduma za kijamii,ujenzi wa miundombinu na miradi muhimu yenye tija kwa jamii kwa mstakabali wa Taifa. Akifafanua zaidi ameeleza dhana ya maendeleo ni kutenda na sio kutumia lugha chafu za matusi wanazotumia wapinzani kujinadi na kuharibu utu wa Watanzania katika kudumisha amani iliyoachwa na hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kuenziwa na Viongozi wengine mpaka sasa kama tunu muhimu ya kudumisha amani na mshikamano kuanzia tulipopata Uhuru kutoka kwa wakoloni pasipo kumwaga damu. Katika hatua hiyo Mhe.Magufuli ametoa siku thelasini na kumtaka naibu Waziri wa Maji Juma Aweso kushughulikia tatizo la maji wilayani Same linalosababishwa na kuchelewa kutekelezwa kwa mradi mkubwa wa Maji unaoanzia katika chanzo Cha nyumba ya Mungu wilayani Mwanga na kupita Same hadi Korogwe. Magufuli amesema mradi huo ulipaswa kukamilika mwaka 2017 na kumtaka mkandarasi kuchukuliwa hatua kali za kisheria pale itakapobainika kuna uzembe uliofanyika kutofikia malengo hayo sambamba na kuendelea kuahidi kuwa atapambana na watumishi wazembe wanaotumia taaluma zao vibaya na kudhorotesha maendeleo ya Taifa . Aidha Magufuli amewetaka wananchi radhi juu ya kutokamilika kwa mradi huo wa maji kwa wakati sanjari na kuwaomba ridhaa ya kumchagua kuwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na kuwachagua wabunge na madiwani wa chama cha Mapinduzi (CCM) ili waweze kuzisimamia vyema rasilimali za Watanzania hivyo wasidanganyike na maneno ya wapinzani kwani hakuna jambo linaloweza kukamilika bila kuwa na mipango na kuwataka wananchi wawe na tafakuri juu ya miradi mingi ya maendeleo iliyofanywa na Serikali ya awamu ya tano na dhamira ya ukuaji wa uchumi.

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 0