المدة الزمنية 29:14

Salama Na Marco Chali Ep 2 | DOKTA Part 1

بواسطة YahStoneTown
38 555 مشاهدة
0
487
تم نشره في 2020/02/12

#YAHStoneTown #SalamaNa #PodCast DOKTA Marco na mimi tumekua marafiki wa miaka mingi na moja kati ya vitu vimetufanya tuwe marafiki ni kufanana kwetu kwa kupenda vitu vya aina moja. Kuanzia teknolojia mpaka muziki, nakumbuka siku ya kwanza kukutana naye, ilikua ni uzinduzi wa kipindi cha Bongo Star Search ambao ulifanyika Much More pale juu, alinifuata akaniambia juu ya mapenzi yake ya kipindi changu cha Planet Bongo enzi hizo na baada ya hapo ikawa ni urafiki ulodumu mpaka leo. Kipindi changu cha Mkasi kilizaliwa kwenye kibaraza cha studio kwa Marco Chali pale MJ RECORDS ambako ilikua ni maskani yetu kubwa mimi na AY. Marco anajua KILA KITU, kuanzia kuendesha baikeli, kutengeneza mabiti, kuandika, kuimba, kuogelea,kucheza basketball kupambana na maisha na ni mwingi wa Imani pia. Amekua akijinyima karibu kila siku ilimradi watu anaowapenda wapate chochote, zaidi kwa familia yake. Katika watu ambao naweza kuwapigia simu nikawaambia sina kitu Marco ni mmoja wapo na anaweza akawa nae ni vivo hiyo ila akanipa mimi na yeye akaenda kutafuta nyengine. Mwaka jana rafiki yangu Mwenyezi Mungu alimbariki mtoto wake wa kwanza, binti, anaitwa Yoy, tabasamu ambalo rafiki yangu analo sikuwahi kuliona likiwa endelevu kama ambavyo toka Yoy amekuja duniani… Mwenyezi Mungu amlindie na amkuzie kwenye misingi iliyo bora na afya njema. Kwenye kikao chetu hiki ingekua inawezekana tungeweza kuongea hata masaa 24, yeah, story zetu zinaweza kufika huko, na siku nyengine tunaweza hata tusiongee kabisa, ikawa mikausho mikali tu ila humu tulipata wasaa wa kumuongelea Yoy, muziki, career yake, Mwenyezi Mungu, Godzilla, mawazo na discipline. Yangu matumaini utapata kadhaa ya kujifunza na kukusogeza. Love, Salama. Listen our Podcast on Boomplay Link boomplay.lnk.to/SalamaNa‬ ‪Spotify Link https://spoti.fi/2Uxr6Cm� �� ‪ApplePodcasts Link https://apple.co/2Ou1bru� �� ‪YouTube Link http://bit.ly/YoutubeSalamaNa Follow: Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown

الفئة

الكلمات

عرض المزيد

تعليقات - 60