KKKT USHARIKA WA KIJITONYAMA : IBADA YA MORNING GLORY THE SCHOOL OF HEALING
MAFUNGO YA SIKU AROBAINI
MADA: TABASAMU TENA- SMILE AGAIN
MAWAZO YA KUFIKIRIKA
"Let your SMILE change the world,
Don't let the world change your SMILE"
(Ruhusu TABASAMU lako libadilishe Ulimwengu; wala usiruhusu ulimwengu ubadilishe TABASAMU lako)
UJUMBE WA LEO : 29/11/2021
MKUKI WA SAULI NA RIZIKI YANGU
Luka 11 : 1 - 4
1 Ikawa alipokuwa mahali fulani akiomba, alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia, Bwana, tufundishe sisi kusali, kama vile Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake.
2 Akawaambia, Msalipo, semeni, Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litakaswe, Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.
3 Utupe siku kwa siku riziki yetu.
4 Utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa sisi nasi tunamsamehe kila tumwiaye. Na usitutie majaribuni lakini tuokoe na yule mwovu.
1 Samweli 18 : 6 - 9, 11 - 12
6 Hata ikawa, walipokuwa wakienda, hapo Daudi aliporudi baada ya kumwua yule Mfilisti, wanawake wakatoka katika miji yote ya Israeli, kwa kuimba na kucheza, ili kumlaki mfalme Sauli; wakatoka na matari, na shangwe, na vinanda.
7 Nao wale wanawake wakaitikiana wakicheza, wakasema, Sauli amewaua elfu zake, Na Daudi makumi elfu yake.
8 Basi Sauli akaghadhibika sana, na maneno haya yakamchukiza; akasema, Wamempa Daudi makumi elfu, na mimi wamenipa elfu tu; kuna nini tena awezayo kupata, isipokuwa ni ufalme?
9 Sauli akamwonea Daudi wivu tangu siku ile.
11 Mara Sauli akautupa ule mkuki; maana alisema, Nitampiga Daudi hata ukutani. Daudi akaepa, akatoka mbele yake, mara mbili.
12 Sauli akamwogopa Daudi, kwa sababu Bwana alikuwa pamoja naye, ila amemwacha Sauli.
1 Samweli 2 : 6 - 9
6 Bwana huua, naye hufanya kuwa hai; Hushusha hata kuzimu, tena huleta juu.
7 Bwana hufukarisha mtu, naye hutajirisha; Hushusha chini, tena huinua juu.
8 Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina Bwana, Naye ameuweka ulimwengu juu yake.
9 Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake; Bali waovu watanyamazishwa gizani, Maana kwa nguvu hakuna atakayeshinda;
Ezekieli 5 : 16
16 hapo nitakapopeleka mishale mibaya ya njaa juu yao, iletayo uharibifu, nitakayoipeleka ili kuwaharibu ninyi; nami nitaiongeza njaa juu yenu, na tegemeo lenu la mkate nitalivunja.
Mhubiri : Mwl Emilian Katubayemo
Kwa maombi na ushauri:
Mch. Dkt. Eliona Kimaro.
Simu :+255655516053, +255754516053
YouTube : Rev. Dr. Eliona Kimaro TV
Barua Pepe: elionakimaro555@gmail.com
الفئة
عرض المزيد
تعليقات - 41
مقاطع الفيديو ذات الصلة على KKKT USHARIKA WA KIJITONYAMA : IBADA YA MORNING GLORY THE SCHOOL OF HEALING 29/ 11 / 2021: