المدة الزمنية 1:1:56

SHIMO NYUMBA YA UHARIBIFU ( DAY ONE) - PASTOR SUNBELLA KYANDO

18 292 مشاهدة
0
293
تم نشره في 2021/11/18

Mithali 15:11 [11]Kuzimu na Uharibifu vi wazi mbele za BWANA; Si zaidi basi, mioyo ya wanadamu? Kuzimu ni eneo ambalo lipo katika ulimwengu wa roho,kwa maana hiyo hata uharibifu pia ni eneo ambalo lipo katika ulimwengu wa roho,na hadi Neno la Mungu linasema kuwa "vi wazi mbele za Bwana" inamaanisha kuwa ni maeneo ambayo kwa macho ya nyama hayaonekaniki. Neno la Mungu linaendelea kuelezea kuhusu huu uharibifu katika kitabu cha Ayubu; Ayubu 26:6 [6]Kaburi li wazi mbele yake, Uharibifu nao hauna kifuniko. Tofauti ya kaburi na uharibifu ni kuwa kaburi baada ya kuzikiwa hufunikwa lakini uharibifu hauna kifuniko,kwa maana nyingine; kama kaburi ni shimo hata uharibifu nao pia ni shimo kasoro tu halina kifuniko,yaani halifunikwi.Ni sawa chupa ya chai,ukimmiminia mtu mmoja ukimaliza utaifunika lakini kama kuna foleni ya watu wa kuwamiminia kwenye vikombe hautoifunika hadi uwamalize.Kwa maana hiyo uharibifu ni shimo ambalo lipo busy sana,watu wanawekwa hapo sana.Kumbuka UHARIBIFU SIO MATOKEO BALI NI ENEO(LOCATION). Na hili jambo lilimtokea pia Daudi; Zaburi 40:1-2 [1]Nalimngoja BWANA kwa saburi, Akaniinamia akakisikia kilio changu. [2]Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu. Mungu baada ya kusikia kilio cha Daudi kitu cha kwanza alichofanya ni kumuhamisha eneo(location) alimokuwemo,yaani shimo la uharibifu.Yeyote anayekuwa ndani ya shimo hakuna kitu atakachokifanya na kikaenda kwa sababu yupo shimoni.Kuna watu kimwili wapo maofisini lakini kiroho wamewekwa kwenye shimo la uharibifu, mshahara wanapata lakini hakuna matunda anayokula kutokana na kazi yake. Biblia inaendelea kusema kuwa "...toka udongo wa utelezi". Kwa maana nyingine hata mtu huyu akijitahidi kutoka kwenye shimo bado atateleza na kuanguka tena,na mara nyingi huumia.Ndio maana kila ambavyo unajitahidi kupiga hatua ndivyo ambavyo unakutana na vitu vya kukuumiza sana na unajikuta unarudi nyuma. Kwa Daudi ilibidi Mungu aingilie kati na kumtoa kwenye hilo shimo, katika sehemu inayofuata tutakuwa na MAOMBEZI na kila shimo la uharibifu ulilowekwa Mungu ataenda kukutoa. UNAWEZA WASILIANA NASI AU KUTUMA SADAKA YAKO KWA NAMBA HII : 0657 173 322 Unaweza kutufuatilia katika mitandao yetu ya kijamii Like our Facebook: https://www.facebook.com/Therealityof ... Follow our Instagram: https://www.instagram.com/realityofch ... Subscribe our YouTube: /channel/UC67L ... Also Subscribe Roc worshippers youtube channel:/channel/UCyVhAzjcFaJH7lxgiMQviGQ and Subscribe Pastor Sunbella Kyando YouTube /channel/UCoBuJc3EbjF6r90ov6B3N0Q

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 41