المدة الزمنية 14:25

GLOBAL HABARI APRIL 13: WAGONJWA WA CORONA WAONGEZEKA, WAFIKIA 49 TANZANIA..

بواسطة Global TV Online
15 346 مشاهدة
0
70
تم نشره في 2020/04/13

GLOBAL HABARI APRIL 13: WAGONJWA WA CORONA WAONGEZEKA, WAFIKIA 49 TANZANIA.. WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wamethibitisha ongezeko la wagonjwa wengine 17 wa Corona na kufanya jumla ya kesi za maambukizi zilizoripotiowa tangu ugonjwa huo uingie nchini kufikia watu 49. Hayo yamebainishwa leo Jumatatu, Aprili 13, 2020 na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, kupitia ripoti ya mwenendo wa ugonjwa wa Corona (Covid-19) nchini na kueleza kuwa wagonjwa 13 wametokea Dar es Salaam na mmoja ametokea mkoani Arusha, Na wengine watatu visiwani Zanzibar na kufanya idadi ya wagonjwa visiani humo kufika 12, ambapo ufuatiliaji wa watu waliokuwa karibu na wagonjwa unaendelea. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wizara ya afya ni kuwa wagonjwa wote wanaendelea na matibabu chini ya uangalizi wa wataalamu wa afya huku Maeneo ambayo ugonjwa huo umeripotiwa ni Dar es Salaam, Zanzibar, Arusha na Mwanza. Aidha serikali inaendelea kusisitiza wananchi kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huu kama inavyotoa taarifa na elimu mara kwa mara kupitia njia mbalimbali na hususan kuepuka misongomano na mikusanyiko isiyokuwa na lazima. UNA HABARI? WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE (+255 784 888982) (+255 676 229628) Email: globaltvbest@gmail.com abbymrisho@gmail.com HABARI MPYA DAILY: http://bit.ly/habarimpya HISTORIA ZA VIONGOZI ZA KUSISIMUA: http://bit.ly/mikasa_ya_kusisimua GLOBAL RADIO TV: http://bit.ly/255globalradio EXCLUSIVE INTERVIEW: http://bit.ly/exclusive_interviews Subscribe Global TV, Channel itakayokupa Habari na matukio ya kipekee nchini Tanzania

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 15