المدة الزمنية 10:2

Fahamu Chanjo anazotakiwa Kupewa Mtoto Mchanga | Je Mtoto Mchanga hutakiwa kupata Chanjo ngapi

بواسطة Dr. Mwanyika
967 مشاهدة
0
20
تم نشره في 2022/01/06

Mara baada ya Mtoto Kuzaliwa hutakiwa Kuchanjwa au kupewa Chanjo kila anapofikilia Umri fulani kama ifuatavyo: 1. Siku ambayo Mtoto amezaliwa hutakiwi kupewa Chanjo ya BCG na Oral Polio Vaccine 0 NB: Endapo Mtoto alikosa Chanjo ya BCG siku aliyo zaliwa anatakiwa Kuchanjwa siku anapokwenda Hospitali. 2. Umri wa Wiki 6 au Mwezi Mmoja Mtoto hutakiwa kupata Chanjo Nne ambapo hupewa: A. Chanjo mbili za Matone (Rotarix Vaccine na Oral Polio Vaccine 1). B.Mbili za kuchoma Pentavalent Vaccine huwa na Mjumuisho wa Chanjo Tano ambazo ni (Diphtheria vaccine, Pertussis vaccine, Tetanus vaccine, Haemophilus influenza vaccine na Hepatitis B vaccine) na PCV-13. 3. Umri wa Wiki 10 au Miezi Miwili na Wiki Mbili. Mtoto hutakiwa kupata Chanjo Nne ambapo hupewa: A. Chanjo mbili za Matone (Rotarix Vaccine na Oral Polio Vaccine 2). B.Mbili za kuchoma Pentavalent Vaccine huwa na Mjumuisho wa Chanjo Tano ambazo ni (Diphtheria vaccine, Pertussis vaccine, Tetanus vaccine, Haemophilus influenza vaccine na Hepatitis B vaccine) na PCV-13. 4. Umri wa Wiki 14 Mtoto hutakiwa kupata Chanjo Tatu. A. Ambapo Mtoto hupewa Chanjo ya Matone (Oral Polio Vaccine). B. Mbili za kuchoma Pentavalent Vaccine huwa na Mjumuisho wa Chanjo Tano ambazo ni (Diphtheria vaccine, Pertussis vaccine, Tetanus vaccine, Haemophilus influenza vaccine na Hepatitis B vaccine) na PCV-13. 5. Umri wa Miezi 9, Mtoto hutakiwa Kuchanjwa Chanjo ya Surua na Rubella ambapo hurudiwa Tena kupewa Chanjo hiyo anapofikisha Miezi 18 au Mwaka Mmoja na Miezi 6. Chanjo na maelezo yake kiufupi: 1. Chanjo ya Polio (Oral Polio Vaccine) ni Chanjo ambayo Mtoto huchanjwa ili kujizuia na Ugonjwa uitwao Poliomyelitis ambao husababishwa na Virusi vya Polio, ambapo mtu akipata Maambukizi huweza Kupooza Mwili hususani Miguu (Mtu mmoja Kati ya Watu 200 huweza Kupooza Miguu na 5% Hadi 10% ya Wagonjwa wanao pooza huweza Kupooza Misuli inayohusika na Upumuaji na kupelekea Kifo. 2. Chanjo ya Kifua Kikuu/TB (BCG vaccine), Aina hii ya Chanjo Watoto hupewa ili kupunguza athari za TB mfano TB inayosambaa Mwili mzima (Milliary TB) au TB ambayo huathiri Kuta zinazo zunguuka Ubongo na Uti wa Mgongo (TB meningitis) 4. Pentavalent Vaccine. Hii hujumuisha Chanjo 5 ambazo ni Chanjo ya Dephtheria, Pertussis, Tetanus, Haemophilus influenza na Chanjo ya Homa ya Ini. 5. Chanjo ya Pneumococcal (PCV-13), Hii ni Chanjo ambayo Mtoto huchanjwa ili kupunguza athari kutokana na Magonjwa yatokanayo na Kijidudu Aina ya Streptococcus Pneumoniae ambaye husababisha Maambukizi kwenye Damu au kwenye kuta zinazozunguka Ubongo na Uti wa Mgongo. 6. Chanjo ya Surua na Rubella, Hizi Mtoto hupewa ili kuzuia Mtoto kupata Ugonjwa wa Surua na Rubella unaosababishwa Paramyxovirus na Virusi vya Rubella kila Mmoja. Nifuatilie kwenye channel yangu kuhusu Mambo ya Ujauzito. /c/DrMwanyika Nifuatilie Instagram kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://www.instagram.com/dr._mwanyika/ Nifuatilie kwenye website hii kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://mamaafya.com/ Nifuatilie kwenye Facebook page kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://www.facebook.com/JapideAfya/ Usisahau kudownload app ya Mama Afya Bora kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://play.google.com/store/apps/details?id=com.wapnum.mamaafyaapp #ChanjoZaKichanga #DrMwanyika #MamaAfya

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 14